Deodati wa Nevers (pia: Dié, Didier, Dieudonné, Déodat, Adéodat; alifariki 679 hivi) alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Ufaransa) kuanzia mwaka 655 hadi 664 alipokwenda kuishi upwekeni.
Anasemekana alianzisha pia monasteri chini ya kanuni ya Kolumbani ambayo imepewa jina lake[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Juni[2].
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search